Mapesbury Clinic - Nasaha kwa wakimbizi wa jinsi tofauti
Maelezo
Clinic ya Mapesbury ni mipango inayo ongoza na inakusudia kuwapatia nasaha
na msaada wa matibabu ukamilifu kwa wakimbizi na waombi wa makaazi (ya amani).
Nasaha na matibu yanapewa na watu waliosomea na wana mafunzo ya juu kutoka
mila na mazoezi tofauti, wengi wao wenyewe walikuwa wakimbizi.
Pia msaada huu inawapatia fursa watu wa nasaha waliyekuwa wakimbizi na wengine
waliye na masomo yanayohitajika na wanazungumza lugha mbali mbali vizuri
nafasi ya kutibu. Hizi nafasi zinasaidiwa kwa maangalizi ya kila wakati
na njia ya kubata masomo zaidi.
Azimio
Azima (kusudi) yetu ya kwanza ni kuwapa wakimbizi na waombi wa makaazi (wa
amani) msaada wa nasaha na matibabu inayo wafaa kwa lugha na mazoezi zao.
Kwa Ajili Ya Nani?
Msaada huu ni wa bure kwa wakimbizi, pamoja na waombi wa makaazi (amani)
na watu ambao wako mbali na nchi zao wenye umri wa miaka 18 na kuzidi wanaokaa
katika mmoja ya mitaa wa London. Hata hivyo, wakimbizi na waombi wa makaazi
(amani) wanaotoka nje ya London hawatonyimwa msaada huu. Inategemeya hali,
Ikihitajika, msaada wa nauli huenda ukapatikana.
Msaada Tunayotowa
Clinic ya Mapesbury inatoa msaada wa nasaha na matibu ukamilifu kwa mazoezi
na malugha tofauti kama Kiarabu ya (Kazkazini ya Africa, Mashariki Kati
na aina zote), Kifaransi, Kifarsi, Kispanish, Kibosni, kitamil, lugha ya
Serbo-Croat, Kikurdish, Kialbani, Kisomali, Kiturkish na Kingereza.
Kadiri na idadi ya lugha zinazotumika kwenya Clinic ina badilika na kuongezeka
baadhi ya wakati. Tafadhali ulizia.
" Pia tunawapa msaada wa kutetea na kupewa maarifa kwa watumiaji wa Clinic
kwa mambo kama ya uhamiaji, msaada wa pesa, pahala pa kukaa, na msaada wa
makaazi (kwa amani). Pia tunawapeleka watumiaji wetu kwa kushauriwa na wenye
ujuzi na kwa kutetewa kwenye hali hizi na nyenginezo. Tafadhali fahamu yakwamba
msaada huu ni kwa ajili ya watu wanaotumia nasaha ya Clinic tu.
" Tunashirikiana na mashirika mengine ili zipatikane njia za misaada mengine
inayohitajiwa na watumiaji wetu.
Unafika Vipi
" Watu wanaweza kuja wenyewe au wanaweza kuletwa na mataktari wao (GPs),
wana afya ama wafanyi kazi wa jamii. Pia Clinic itakubali watu wanaoletwa
na mashirika ya umati na yaliojitolea. Mafomu ya kujaza zinaweza kupatikana
katika Clinic, kutoka kwenye ukurasa wetu wa Internet, au tunaweza kupokea
mafomu mengine yaliyojazwa kama inavyotakiwa.
" Mafomu yakifika tu, watumiaji wataarifiwa. Baadae inaweza kufika miezi
mitatu kabla ya kuarifiwa lini utaulizwa masuali.
" Haya maswali yatatuwezesha kufahamu msaada wa nasaha au matibabu ambayo itakufaa na tunaweza kukupatiya. Kama Nasaha haifai, mtumiaji na mtu ambaye aliemleta watajulishwa kwa maandishi.
Baada ya mkutano (wa maswali)
Nasaha au matibabu yataanza mara tu patapopatikana nafasi. Mpaka hapo, watu
watakuwa kwenye orodha ya kuongojeya na wataambiwa muda utakao kuwa.
Watumiaji wataweza kutumiya msaada wa kutetewa na Clinic na kupewa maarifa
ikiwa wanahitaji misaada mengine kama zile zinazohusu makaazi.
Nasaha inatolewa kwa wiki mara moja, muda wa mara kumi na mbili kwa kawaida.
Ikibidi nasaha ama tibabu yanaweza kutolewa kwa muda mrefu lakini inategemeya
hali ya watu.
Misaada ambayo hatutowi
Clinic ya Mapesbury haitowi misaada ya ghafla; watumiaji wataangiliwa baada
ya kufanya miadi tu.
Msaada hii haifai kwa wagonjwa wanayo ugonjwa wa akili au hivi sasa wana
matatizo ya kutumia zaidi madoroga (madawa ya unga) ama kunywa ulevi. Wenye
matatizo haya watapelekwa kutafuta misaada kwa wana maarifa wengine wakipatikana,
wapewe shauri inayo wafaa.
Siri
Maandishi na maelezo mengine tulizopata kwa watumiaji wetu yatawekwa kwa
mahala pa siri sana kwa maaila, marafiki na watu wengine wote wasijuwe.
Tutaweza kuwaonyosha watu wengine baada ya kupata ruhusa ya maandhishi kutoka
kwa mtumiaji aliehusika tu. Ikibidi twende kinyume na sharia (ya siri) maelezo
yatatolewa mwanzo wa mkutano wa nasaha.
Wakati wa kufunguwa na masuali
Kuletwa
Wafanyi kazi wanapatikana Jumanne mpaka Ijumaa kutoka saa
10:00 asubuhi mpaka 5:30 alasiri na Jumamosi kutoka
10:00 asubuhi mpaka 2:00 adhuhuri.
Nasaha
Pia misaada inaweza kupatikana baada ya afisi kufungwa.
Wenye vilema wanaweza kuingia ndani ya jengo letu na magari yao.
Maswali
Ukihitaji habari nyengine au una maswali piga simu kwa Klinic 020 7644 6250
au angalia ukurasa wetu wa Internet www.mapesburyclinic.org.uk
Download PDF version here